Personal Saving Account

Kama unahitaji kuwekeza pesa zako kwa ajili ya kwenda likizo, fungate, kununua gari, vifaa mbalimbali na kulipia ada ya shule basi DCB Savings Akaunti ni mahsusi kwa ajili yako.
 
Akaunti ya Shilingi / Local Currency Account       Fedha za kigeni / Foreign Currency Account
Sifa na manufaa ya akaunti hii ni:

» Kiwango kidogo cha kufungua akaunti: Unahitaji Sh. 5,000 tu kufungua akaunti hii na salio la Sh. 20,000 kwenye akaunti yako. 

» Utapata riba nzuri kwa mwezi kwa salio linaloanzia Tsh. 50,000 au zaidi.
» Utapata ATM kadi ya UmojaSwitch, yenye mtandao wa mabenki zaidi ya 25 nchini, DCB ikiwa ni mwanachama.
» Urahisi wa kupata mkopo kwa kutumia amana yako kama dhamana.

Viambatanisho vinavyohitajika kwa ajili ya kufungua Akaunti:
- Pasipoti, kitambulisho cha kupiga kura, leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi.
- Picha mbili za paspoti za rangi.
- Uthibitisho wa sehemu unayoishi: Mojawapo ya vifuatavyo; barua kutoka serikali za mitaa, Mwanasheria, Hati ya nyumba, Mkataba wa kupanga nyumba au bili ya umeme au maji yenye anwani ya mahali unapoishi.
- Kama si mtanzania uwe na hati ya kusafiria na hati ya kufanya kazi nchini kutoka uhamiaji.

Fungua akaunti yako ya akiba kutoka DCB sasa unufaike!

  Sifa na manufaa ya akaunti hii ni:

» Kiwango kidogo cha kufungua akaunti: Unahitaji USD/EURO/GBP 5 tu kufungua akaunti hii na salio la  USD/EURO/GBP 20 kwenye akaunti yako. 

» Utapata riba nzuri kwa mwezi kwa salio linaloanzia USD/EURO/GBP 50 au zaidi.
» Urahisi wa kupata mkopo kwa kutumia amana yako kama dhamana.

Viambatanisho vinavyohitajika kwa ajili ya kufungua Akaunti:
- Pasipoti, kitambulisho cha kupiga kura, leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi.
- Picha mbili za paspoti za rangi.
- Uthibitisho wa sehemu unayoishi: Mojawapo ya vifuatavyo; barua kutoka serikali za mitaa, Mwanasheria, Hati ya nyumba, Mkataba wa kupanga nyumba au bili ya umeme au maji yenye anwani ya mahali unapoishi.
- Kama si mtanzania uwe na hati ya kusafiria na hati ya kufanya kazi nchini kutoka uhamiaji.
 
​Fungua akaunti yako ya akiba kutoka DCB sasa unufaike!