Taarifa Ya Mkutano Mkuu 2016

TAARIFA INATOLEWA KWAMBA, Mkutano Mkuu wa Kumi na Nne wa Wanahisa wa DCB Commercial Bank Plc, utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 28 Mei, 2016, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga, Dar-es-Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi.
 
Agenda
1.         Kuridhia Agenda za Mkutano.
2.         Kuthibitisha kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa Kumi na Tatu wa Wanahisa uliofanyika tarehe 23 Mei, 2015.
3.         Kupokea Na Kuridhia Utekelezaji wa Yatokanayo Na Mkutano Mkuu Wa Kumi na Tatu uliofanyika tarehe 23 Mei, 2015.
4.         Kupokea na Kuridhia Taarifa ya Wakurugenzi na ya Hesabu zilizokaguliwa za Mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba, 2015.
5.         Taarifa kwa Mujibuwa Agizo la Benki Kuu
6.         Kuridhia na Kupitisha Gawio kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba 2015.
7.         Kujadili na Kuridhia Mabadiliko ya Vifungu vya Katiba ya Kampuni
Kupitisha azimio la kurekebisha kanuni za Katiba ya Kampuni kama ifuatavyo:
a.        Kuingiza kifungu kipya namba 3(a)viii kitakachosomeka ifuatavyo:
“kufanya kazi kama wakala wa bima kwa niaba ya Serikali yoyote au mamlaka nyingine na kwa ajili ya vyombo vya umma na vya watu binafsi na mtu mmoja”.
 
b.         Kuingiza kifungu kipya namba 51(4) kitakachosomeka kama ifuatavyo:
Mkurugenzi aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni namba 51(1) na 51(3), anastahili kuteua mwajiriwa wa Mwanahisa kuwa Mkurugenzi Mbadala”
 
c.         Kurekebisha kifungu namba 52(7) kitakachosomeka kama ifuatavyo:
“Mkurugenzi atakayeteuliwa na Wanahisa Waanzilishi au Mwanahisa wa Kitaasisi atawasilishwa Benki Kuu kwa uchambuzi makini baada ya kuthibitishwa na Mkutano Mkuu”
8.         Kuthibitisha na Kuchagua Wajumbe wa Bodi
9.         Kupokea na Kuridhia pendekezo la Malipo ya Ada kwa Wajumbe wa Bodi kwa mwaka 2016
10.      Kuteua Mkaguzi Huru wa Hesabu kwa mwaka 2016.
11.      Kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu Ujao.
MAELEZO
1.     Mwanahisa atakayehudhuria Mkutano Mkuu atatakiwa kujigharamia mwenyewe na aje na Hati ya Hisa iliyotolewa na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam pamoja na kitambulisho chake, kadi ya kupiga kura au hatiyakusafiria au kitambulisho cha kazi. Vitabu vyenye Taarifa ya Hesabu ya Mwaka 2015 pamoja na fomu ya mwakilishi mbadala (proxy) vitapatikana ofisi za Makao Makuu zilizoko jengo la DCB, Magomeni Mwembechai na katika matawi yote na ofisi za madalali wa Soko la Hisa la Dar-es-Salaam kuanzia tarehe 16 Mei 2016.
 
2.     Mwanahisa anayestahili kuhudhuria na kupiga kura lakini akashindwa kuhudhuria kikao, anaweza kuwasilisha Jina la Mbadala wake (Proxy) kwa Katibu wa benki kabla ya saa 8.00 mchana Alhamisi ya tarehe 26 Mei 2016 katika ofisi za Makao Makuu zilizoko jengo la DCB, Magomeni Mwembechai. Kwa makampuni, fomu inapaswa kuwa katika lakiri ya kampuni mwanahisa.
 
3.     Kwa idhini ya Benki Kuu na azimio la Wanahisa, Bodi ya Wakurugenzi wa benki inapendekeza gawio la Sh. 22 kwa hisa kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba 2015, lilipwe kwa wanahisa, sambamba na sera ya benki yetu ya kulipa asilimia 50 ya faida baada ya kodi.
 
 
 
4.     Hisa za Benki zilianza kuuzwa kama ifuatavyo:
Mwanzo wa mauzo ya hisa pamoja na haki ya gawio              - tarehe 5 Mei 2016
Mwisho wa mauzo ya hisa pamoja na haki ya gawio               - tarehe 25 Mei 2016
Mwanzo wa mauzo ya hisa bila haki ya gawio             - tarehe 26 Mei 2016
Kufungwa kwa Rejesta ya Wanahisa                                      - tarehe 31 Mei 2016
Malipo ya gawio                                                                   - kuanzia tarehe 15 Juni 2016
 
5.     Mapendekezo ya Wanahisa ya wasilishwe kwenye ofisi za Makao Makuu zilizoko Jengo la DCB Magomeni Mwembechai kabla ya saa 8.00 mchana siku ya Jumatano tarehe 25 Mei 2016.
 
KWA IDHINI YA BODI,

Caroline Mmasi Mduma
KatibuwaKampuni
Aprili, 2016.